SERIKALI IPIGE JEKI WANABARINGO KATIKA MASUALA YA USALAMA

  

Na Janelle okongo.

Published in Taifa leo on 15th, March 2022

Visa vya utovu wa usalama vinaendelea kukithiri mipaka maeneo ya Baringo na kupelekea wakaazi wake kujawa na hofu tele kuhusu maisha yao.

Wengi wa wale wanaoishi Baringo wamekosa subira na kuchukua hatua ya kugura makao yao rasmi pamoja na mifugo wao ili kutafuta mahali salama pa kujisitiri huku wakiomba serikali iwanusuru kutoka kwa masaibu wanayopitia. Hali hio iliwakosesha amani watahiniwa wa mtihani wa Kitaifa wa KCPE waliokuwa wanaishi maeneo hayo. Hata hivyo, hivi majuzi kumetokea mashambulizi ya mkuu wa polisi na mwenzake Kule kapkechir waliofyatuliwa risasi na maharamia wasiojulikana. Takriban watu ishirini na tatu wamepoteza uhai wao tangu shambulizi hilo kutukia.

Wakaazi wa Baringo wanalilia usalama wao. Iwapo polisi wanauwawa sembuse mwananchi wa kawaida asiye na ujuzi wala kifaa cha kukabiliana na maharamia hao? Waziri wa usalama ashirikiane na serikali ili kupeleka majeshi eneo la Baringo kushughulikia usalama na wakaazi wahamasishwe namna ya kushirikiana na polisi ili kumaliza janga hili sugu lisienee zaidi.

Janelle


Comments

Popular posts from this blog

EXECUTE EMPLOYMENT LAWS GOVERNING PWDS

GHARAMA YA PEMBEJEO IPUNGUZWE MSIMU WA UPANZI